Posts

Image
    “DAKIKA 180 GOLGOTHA” Amithay Hezekiah Kuhanda (PhD) UTANGULIZI  Maadhimisho ya Sikukuu ya Pasaka 2026 yananifanya kutafakari upya tukio la ukombozi wa mateka (waliotekwa) lijulikanavyo kama ‘Dakika 90 Entebbe’. Tukio hili la kweli la uokoaji wa mateka 103 wa kiyahudi lilitokea tarehe 4 July 1976. Anasimulia Stevenson (1976) [1] kuwa makomandoo wa Israeli walisafiri umbali wa kilomita 4000 kuja kuwakomboa ndugu zao waliokuwa wanashikiliwa na magaidi saba (7) katika uwanja wa ndege Entebbe. Mateka hao walichambuliwa na kushikiliwa kutoka kwenye ndege kubwa ya abiria (Air France, Flight 139) iliyotekwa ikiwa Ugiriki na kuelekezwa Libya, na baadaye Entebbe nchini Uganda. Makoandoo 100 wa Israeli, walioendesha ‘operesheni thunderbolt’, walifanikiwa kuwaua magaidi wote saba, askari kadhaa wa jeshi la Uganda, na kuwakomboa mateka wote, isipokuwa mateka mmoja aliyekuwa amepelekwa hospitali kutibiwa. Tukio la ‘operation thunderbolt’ lilichukua muda mfupi, dakika 90. ...

NDOA NA FAMILIA

Image
  Mpendwa msomaji! Kupitia blog hii tunatamani kuanza kujifunza masuala yanayohusiana na ndoa. Kabla ya kuzama katika mada hiyo nyeti, natamani tuanze kwa kuangalia kanuni muhimu za kufasiri (kutafsiri) maandiko. Kanuni mojawapo inajulikana kama Exgesis . Kanuni hii hutoa hutafsiri kulingana na muktadha wa maandiko husika. Katika kanuni hii, msomaji huanza kwanza kutathmini kama maandiko hayo yamo katika Agano la Kale au katika Agano Jipya. Vile vile kanuni hii inamtaka msomaji kutathmini maandiko kulingana na maandiko mengine yanayozunguka kifungu hicho (muktadha wa karibu) na, kulinganisha na mafundisho yote ya Biblia (muktadha wa kina). Adeyemo na wenzake (2006 uk 2434) wanatuambia kuwa kadiri kifungu kinachosomwa kinavyokuwa kidogo, ndivyo uwezekano wa makosa ya kutafsiri unavyoongezeka. Maandishi mafupi kwa kawaida huwa na maelezo machache kuhusu mada ya jumla ya kifungu kikubwa. Vile vile, ni muhimu kila tamko lieleweke kulingana na maana yake ya asili katika muktadha wa ...